Taarifa ya Habari 16 Agosti 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kiongozi wa upinzani Peter Dutton ame shtumiwa kwa ubaguzi na kuchochea mgawanyiko na baadhi ya wabunge ambao wame kosoa wito waku wazuia wa Palestina ambao wame kwama Gaza kuingia Australia.


Takriban viza elfu tatu zime tolewa kwa watu wanao kimbia vita Gaza tangu Oktoba 7, wakati zaidi ya viza elfu saba zime kataliwa. Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amedai wapalestina wanao unga mkono Hamas, wanaweza sababisha hatari kwa kwa usalama wa Australia. Mbunge huru Zali Steggall amesema Bw Dutton, anataka sema waathiriwa wama bomu ni magaidi.

Wa Australia wame shauriwa wachunguze vifaa vyao vinavyo jumuisha simu za zamani na vifaa vya matibabu, kuhakikisha vita endelea kufanya kazi baada ya mtandao wa 3G kustaafishwa. Tarehe yaku staafishwa kwa mtandao huo ilikuwa mwisho wa Agosti ila, sasa muda huo ume sogezwa mbele kwa miezi mingine mbili baada ya wanaharakati kuonya kuwa wa Australia wengi hawako tayari kwa mageuzi hayo.

Benki Kuu ya Australia inatetea uamuzi wayo kwa viwango vya riba wakati familia na biashara zinapitia wakati mgumu kupitia mfumuko wa bei na kiwewe cha deni yakununua nyumba. Gavana Michele Bullock na timu yake walifika mbele ya kamati ya uchumi ya nyumba yawa wakilishi jana Alhamisi, kwa tathmini yao ya mara kwa mara.
Katika mwezi wa Agosti, benki hiyo iliweka kiwango cha hela taslim kwa asilimia 4.35, iki dokeza mfumuko wa bei kama sababu yakuto punguza riba.

Serikali ya Rwanda imetia saini mkataba wa maelewano siku ya Jumatano na kampuni ya Kimarekani ya Nano Nuclear Energy kwa ajili ya ujenzi wa vinu vidogo vya nyuklia (SMR), Mamlaka ya Nishati ya Atomiki ya Rwanda (RAEB) imetangaza.

Shirika la afya duniani, WHO, limetangza ugonjwa wa MPOX kuwa janga la dharura la kimataifa la afya, kwa mara ya pili kwa kipindi cha miaka 2, hasa baada ya mlipuko wa ugonjwa huo katika taifa la DRC na ambao umesambaa kwa mataifa jirani, kama vile Burundi, Uganda na Kenya. Haya yanajiri wakati huu nchi ya DRC ikiwa ndio imeathirika zaidi na maambukizo ya Mpox, kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa mjini Bukavu kikiendelea kuwahudumia wagonjwa.

Mazungumzo hayo yaliyoanza nchini Uswisi, yanahudhuriwa tu na wanamgambo wa RSF, kundi hasimu kwa jeshi la Sudan. Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani Antony Blinken, kwa njia ya simu ametoa wito huo kwa kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abddel Fattah al-Burhan. Msemaji wa wizara hiyo ya kigeni ya Marekani Vedant Patel amesema Blinken katika mazungumzo yake ya simu na al-Burhan, amemsisitizia umuhimu wa kushiriki kwake na haja ya pande zote mbili kusitisha mapigano na kuhakikisha mamilioni ya watu wanaotaabika wanafikiwa na misaada ya kiutu.

Share