Taarifa ya Habari 13 Agosti 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Viongozi wa Marekani na Uingereza wanaweza jiondoa katika makubaliano ya manowari yaliyofanywa na Australia chini ya mpangilio wa AUKUS, kwa kutoa onyo la mwaka mmoja tu kulingana na hati mpya ya ushirikiano huo.


Chini ya makubaliano yaliyorekebishwa, Australia itawafidia washirika wake kwa chochote watakacho poteza au, jeraha linalo husiana na kuhifadhi takataka ya nyuklia.
Hati mpya zinazo husiana na ushirikiano zili wasilishwa bungeni jana Jumatatu 12 Agosti. Hati hizo zina onesha makubaliano ya pande tatu yata salia hadi Disemba 2075.

Waziri mpya wa shirikisho wa makazi amesema kipaumbele chake, niku pata nyumba nyingi zaidi kwa wa Australia. Clare O'Neil alichukua wadhifa huo kama sehemu ya mageuzi katika baraza la mawaziri, yaliyo sababishwa na kujiuzulu kwa mawaziri Linda Burney na Brendan O'Connor. Hakuna njia iliyo wazi kupitia bunge kwa miswada mbili ya serikali kuhusu nyumba, miswada hiyo ni ya Jenga ku kodi na Kusaidia walipa kodi.

Upigaji kura wa mapema ume anza katika Wilaya ya Kaskazini, kabla ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo tarehe 24 Agosti. Wapiga kura wata wachagua wanachama 25 wa bunge watakao hudumu kwa muda wa miaka minne. Chama cha Labor kina dhibiti viti 14, chama cha Country Liberal Party kina viti saba na upinzani utahitaji kushinda angalau viti 13 ili kiweze kuongoza chenyewe. Wapiga kura kwa sasa wanaweza piga kura kwa simu au kupitia chaguzi yakutuma kura zao kwa posta. Uhalifu, gharama yamaisha na nyumba ni vitu vime ibuka kama maswala muhimu ya uchaguzi. Shirika la Human Rights Law Centre lime omba vyama vyote katika wilaya ya kaskazini, zi heshimu sera zao zakupunguza viwango vya kufungwa kwa watu wa asili.

Polisi wamesema hakuna tisho la ziada kwa umma, baada ya ajali ya helikopta katika paa ya hoteli mja mjini Cairns, Kaskazini Queensland. Rubani wa helikopta hiyo alikuwa peke yake, ali fariki katika ajali hiyo na haja tambulia rasmi. Huduma za dharura zilikimbilia katika eneo la ajali kabla ya saa nane usiku.

Polisi wa Tanzania Jumapili walipiga maarufuku mkutano uliokuwa umepangwa wa vijana wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, wakiwatuhumu kupanga maandamano yenye vurugu. Tawi la vijana wa Chadema lilikuwa limetangaza siku ya Jumamosi kwamba vijana wapatao 10,000 walitarajiwa kukutana katika mji wa kusini magharibi wa Mbeya kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana leo Jumatatu chini ya kauli mbiyu “chukua udhibiti wa mstakabali wako.” Maafisa wa chadema wamelaani uamuzi huo, na kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati, wakiituhumu polisi kwa kujaribu kuzuia misafara ya magari inayoelekea Mbeya na kuwakamata baadhi ya vijana.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema amani ya kikanda ni "kipaumbele chake" katika kukabiliana na mzozo unaoendelea kwenye nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Huku mzozo ukiendelea kufukuta baina ya nchi hizo. Kagame ameyasema hayo mbele ya viongozi kadhaa wa nchi na mataifa mengine ya Afrika ambao walihudhuria sherehe za kuapishwa kwake mjini Kigali. Kiongozi huyo, ambaye anatajwa kuiongoza Rwanda kwa mkono wa chuma tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ,aliahidi kulinda amani, mipaka ya taifa hilo na kuleta umoja wa kitaifa. Matokeo ya uchaguzi wa Julai 15 ambayo yalimrejesha madarakani Rais Kagame kwa kupata ushindi wa asilimia 99.18 yanashutumiwa vikali na wanaharakati wa haki za binaadamu wakisema ni ukumbusho tosha wa utawala dhalimu nchini Rwanda. Wagombea wawili tu ndio walioidhinishwa kugombea dhidi yake, huku wakosoaji kadhaa mashuhuri wakizuiliwa.

Idadi ya watu waliofariki nchini Uganda kutokana na mkasa uliotokea katika eneo la kutupa taka la Kiteezi imefikia 23, wakati rais Yoweri Museveni akiagieza uchuguzi kufanyika kutokana na mkasa huo. Ni mkasa uliotokana na taka kuangakia eneo la maakazi ya raia, shughuli za uokozi bado zinaendelea kutafuta manusura katika eneo la mkasa. Ripoti zaidi zinasema miundo mbinu ya kuzuia takataka hiyo, katika eneo hilo ilivunjika Jumamosi asubuhi na kusababisha maporomoko katika eneo hilo. Eneo la Kiteezi, tangu mwaka 1996 limekuwa likitumiwa kama sehemu ya kutupa takataka kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Kampala. Vyombo vya habari vya ndani vimechapisha zinazoonyesha watu, nyumba na mifugo wakiwa wamezikwa katika takataka hizo kaskazini mwa jiji la Kampala katika wilaya ya Kiteezi.







Share