Bei za petroli duniani zime chochewa na ongezeko la vurugu katika ukanda wa mashariki ya kati ila, mweka hazina Jim Chalmers amesema bei endelevu za juu zitakuwa na madhara kwa familia na uchumi. Mweka hazina amekadiria kuwa kila ongezeko ya senti 10 katika bei ya petroli itaondoa asilimia 0.1 kutoka pato lataifa la Australia nakuongeza takriban asilimia 0.4 katika mfumuko wa bei.
Waziri wa elimu wa shirikisho Jason Clare amewasilisha muswada bungeni, ambao utasaidia serikali ya madola kuongeza mchango wayo katika uwekezaji wa elimu ya umma. Katika juhudi yakuwekeza kwa usawa zaidi shule za umma nakupiga jeki idadi ya wanafunzi wanao hitimu kutoka shule za sekondari, makubaliano ya 10-year Better and Fairer Schools yanapendekeza kuongeza mchango wa serikali ya shirikisho kwa shule za umma nakutoa hela zakusaidia katika mafunzo ya ziada. Muswada huo unafuata mashauriano yaliyo fanywa kwa makubaliano ambayo yame kwama kwa miezi kadhaa.
Kongomano la pande mbili za mpaka lina endelea kwa swala la mitandao yakijamii na matumizi ya vijana. Majadiliano katika kongamano la siku mbili kati ya serikali za New South Wales na Kusini Australia, yanatarajiwa kulenga maswala ya marufuku ya vijana badala ya kama marufuku hayo yata wasilishwa. ReachOut ni shirika linalo toa huduma ya afya ya akili kwa vijana, shirika hilo limesema kuondoa mtandao wa kijamii kunaweza zuia upatikanaji kwa kile ambacho kimekuwa msaada muhimu kwa kizazi cha vijana.
Ajali ya boti iliyotokea kwenye Ziwa Kivu tarehe 3 Oktoba imewauwa watu 34, kulingana na hesabu rasmi ya serikali iliyotolewa Alhamisi. Miili ya watu 11 kati ya 34 waliothibitishwa kufariki ilizikwa kwenye shamba la makaburi la makao, wilayani Nyiragongo, umbali kidogo kutoka mji wa Goma. Hata hivyo, gesi inayoendelea kuwa kwenye Ziwa Kivu imekuwa kikwazo katika juhudi za kuopoa miili mingine inayozaniwa kuwa imekwama kwenye mabaki ya boti iliyojaa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu Tanzania yametoa wito kwa mamlaka kutupa jicho na kufuta adhabu ya kifo ambayo haijatekelezwa kwa zaidi ya miaka 30 huku wafungwa wake wakiendelea kusubiri adhabu hiyo. Mashirika hayo ambayo Alhamis yalikusanyika pamoja kama sehemu ya kuadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani yanasema adhabu hiyo siyo tu kwamba inatweza utu lakini pia inakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu. Licha ya Tanzania kuwa na makosa ya aina tatu yanayotoa adhabu ya kifo, ambayo kuua kwa kukusudia, uhaini pamoja na yale ya kijeshi, hata hivyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa hakuna mfungwa yoyote aliyenyongwa hali ambayo inawapa msukumo watetezi wa haki za binaadamu kuona kutokokuwa na haja ya kuendelea na adhabu hiyo. Wanaharakati wanataka serikali kuchukua mkondo mwingine na kuleta adhabu mbadala ambayo wanasema itazingatia utu wa binadamu na kuheshimu mikataba ya kimataifa.
Bunge la Seneti nchini Kenya litaanza kujadili hoja ya kumuondoa madarakani Naibu wa rais Rigathi Gachagua siku za Jumatano na Alhamisi wiki ijayo siku moja baada ya Baraza la Wawakilishi kupiga kura ya kumuondoa madarakani. Bunge zima la Seneti litachunguza mashtaka dhidi ya Gachagua na kusikiliza ushahidi kutoka pande zote.
Wabunge 281 nchini Kenya waliunga mkono hoja ya kumuondoa madarakani naibu wa rais Rigathi Gachagua siku ya Jumanne. Kiwango kilichowekwa na katiba ni angalau wabunge 233.
Australia yajinusuru katika dimba ya Adelaide Oval, baada yawa China kuzua tumbo joto katika mechi yakufunzu kwa kombe la dunia la FIFA na wagiriki wavunja ukame wakushinda nchini Uingereza na waandalizi wa michuano ya wazi ya Australia katika mchezo wa tennis watumai Nick Kyrgios atashiriki katika michuano hiyo mwakani.