Mtoto wako ananyanyaswa shuleni au mtandaoni? Hatua muhimu unastahili chukua

Left Out

Source: Getty / Getty Images

Kutoa mazingira salama na jumuishi ni dhamira ya msingi ya kila jumuiya ya shule ya Australia.


Ila wazazi wanastahili fanya nini mtoto wao anapo nyanyaswa shuleni? Na ni hatua gani wana stahili chukua kama unyanyasaji huo unafanyika mtandaoni?

Kusaidia kujibu maswali haya, tume waomba wataalam katika elimu, saikolojia na unyanyasaji wa mtandaoni majibu kwa ushauri na maarifa ya hivi karibuni.

Tabia ya unyanyasaji huja katika umbo tofauti na viwango vya madhara. Bila kujali hali, wataalam wamesema haistahili chukuliwa kirahisi.


Share