Hoja hiyo imekuwa kero kubwa kwa wanajumuiya hao na licha ya maombi mengi kwa mamlaka husika hapajawa mabadiliko yoyote.
Katika mazungumzo maalum aliyo fanya na SBS Swahili, Balozi wa Kenya nchini Australia Mhe Dkt Wilson Kogo, alitoa wito kwa mamlaka husika iwa ondolee wa Kenya sharti hilo pamoja naku tambua taifa hilo kama nchi inayo zungumza Kiingereza.
Mhe Dkt Kogo alifunguka pia kuhusu uwakilishi mwingine anao wafanyia wakenya, nchini Australia. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.